![]() |
Incubators ni Mashine zinazo tumika kutotoreshea viumbe mbali mabali hasa Ndege.
AINA ZA INCUBATORS
Forced Air IncubatorStill Air Incubators
FORCED AIR INCUBATOR
Forced Air Incubators ni mashine yenye Feni kwa ajili ya kutawanya joto ndani ya incubators
STILL AIR INCUBATORS
Hii ni mashine siyo kuwa na fane
IPI NZURI?
Inashauriwa
kutumia/kununua Forced Air Incubators ndo bora kabisa na haitakusmbua
na hatahivyo kwa incubator kubwa karibia zote ni Fored air, na mara
nyingi ndogo ndo still air
AINZA INCUBATOR KWENYE OPERATION
Manual
Automatic
MANUAL INCUBATORS
Hizi hutumia mikono katika kugeuuza mayai na katika maswala mengine kama kucontro joto na kazalika
AUTOMATIC INCUBATORS
Hizi
hujiendesha kama Computer, kila kitu hufanywa automatically so kazi za
manual hupunguza sana, Ukiwa na Incubnator Automatic na ikawa na sehemu
ambayo inajiongeza maji automatically basi inaweza hata kata wiki bila
kuchungulia mashine yako na ikawa inapiga kazi bila tatizo.
NI IPI NZURI?
Kwa
kweli kwa maisha ya sasa inahitajika Automati Incubators ambayo
haitahitaji wewe kuwepo mara kwa mara katika ku contro mashine, Ingawa
kuna wakati Manual inahitajika kuliko Automatic na kuna wakati Automatic
inahitajika kuliko manual
NB: Automatic nyingi zina
manual, yaani kuna sehemu ya kushft kwenda manual, ila manual karibia
zote hazina sehemu ya kushift kwenda automatic
ILA ZOTE ZINAFANYA KAZI KWA UFANISI SAWA, TOFAUTI MOJA NI AUTOMATIC NA NYINGINE NI MANUAL.
MAMBO MUHIMU SANA KWENYE INCUBATORS
Aina ya incubators, Model of operation, Manufacturer, Nishati inazo tumia na nishati mbadala.
MANUFACTURE
Incubator
nyingi za nje ni nzuri sana, Kuna za Italy, Denmark, Uk, China, USA,
India, South Africa Trukey na kazalika na bei zinatofautiana. Na utaona
kwamba Incubator kama za Uk, South, USA, Italy ni very expensive compare
na za kutoka China au India. Ila bei kutofautiana sana sio ishu na kama
mnavyo jua China wao wna Policy yao kuhusu Internatinal Trade that is
why.
Mashine nza Ndani ya Nchi nazo zipo nzuri na zipo
zingine ni vimeo ila watengenezaji wanatakiwa kuwekeza zaidi kwenye
Utafiti na si kujikita kwenye mauzo, inatakiwa kuboreshwa zaidi na zaidi
ili ziwe na viwango vizuri
SOURCE OF ENERGY
Incubators
karibia zote zinatumia Umeme kama source namba moja na jua, makaa ya
mawe au gas kama source namba mbili, ingawa zipo za mafuta ya taa pia
kama source No 1
ALTENATIVE SOURCE OF ENERGY
Kila
aina ya mtengenezaji ana source yake ya altenative energy, zipo za Gas,
zipo za umeme jua na zipo za mvuke wa maji na zipo za mafuta ya taa, na
zipo za makaa yam awe.
ALTENATIVE SOURCE NZURI
Kwangu
mimi Incubators ambazo altenative source of energy ni Mvuke wa maji
nimetokea kuzipenda sanaHapa umeme ukikatika unaunga pipe kwenye Mashine
na unakuwa na birika special na unaiweka jikoni maji yanachemka na
mvuke unapita hadi kwenye incubators, ni source nzuri sana, Hata jua
nayo ni source poa
ILA BADO SOURCE YA JUA AU GAS INAKUWA NI ALTENATIVE NZURI SANA.
MATATIZO YA INCUBATORS
Incubators
nyingi zina shida moja kubwa sana, Incubators inaweza ikaharibika na
wewe usiwe na habari kabisa na mpaka uje kushutuka ilisha haribu mayai
yote na hilo ni tatizo kubwa sana
MFANO:
Heating
tube zinaweza kufa na wewe usijue kabisa, na ukija shtukia ilishaharibu
kila kitu Humidity Tube inaweza kufa na wewe usijue na ukija shitukia
ni balaa Eggs turning inaweza kufa na usitambue hata siku mbili Humidity
sensor na temperature sonsor zinaweza kufa na wewe usijue chochoteNa
mara nyingi kinaweza kufeli kifaa kimoja za vingine viakendelea na kazi
bila shida ila ikawa ndo kama hivyo, Mfano Mashine inaweza kuwa imekufa
Humidity tube, na hapo inaweza endelea kufanya kazi na some time ni
vigumu sana kugundua. Na tofauti na mitambo kama gari, Incunator inapo
haribika huku ukiwa umeweka mayai ni balaa tupu, kama huna mashine
nyingine ndo inakuwa imeharibu mayai yote.
KUKATIKA KWA UMEME
Endapo
umeme utakatika na ukatumia Gas, au mafuta ya taa au makaa yam awe kama
source nyingine ni lazima ugeuze mayai kwa mkono, na hapa tatizo liko
kwamba ile mashine haiwezi kukubali kugeka ni lazima ubonyeze sehemu ya
kubadilisha kutoka automatic kwenda manual. HAPA NDO HUWA KUNA KAZI PEVU
Na
Mwisho ni kuhusu uendeshaji wa Incubators, Mara nyingi uendeshaji nao
ni tatizo kubwa sana hasa kwenye kurekebisha joto na unyevu lazima
zitofautiane kulingana na maeneo au vipindi Fulani, Joto na wakati wa
Baridi kali
...................................................................................................................................
