• Ugonjwa huu hutokea muda mfupi baada ya ng’ombe kuzaa (< 72 hrs).
• Neno “MILK FEVER” halina uhusiano na sababisho la ugonjwa wenyewe.
– Kuacha kula.
– Kutokua mchangamfu (dullness)
– Kupindisha shingo upande
– Joto la mwili la kawaida (lakini muda ukizidi kupita joto la mwili hushuka) matatizo mengine kama haya hujulikana kama DOWNER SYNDROME
– Ng’ombe mwenye dalili hizo hudungwa sindano yenye dawa iitwayo Calcium borogluconate
KINGA
– Hakikisha ng’ombe mwenye mimba anapewa chakula chenye virutubisho vya madini na vitamin hasa miezi miwili kabla ya kuzaa (dry period). Virutubisho hivyo ni kama Farmers Super Lick, Farmers mineral block au Oligovit® injection, Chokaa, Unga wa mifupa, unga wa dagaa, majani mabichi n.k.
• “Downer Cow Syndrome” huoanisha matatizo yafuatayo:-
– Uchunguzi wa makini unahitajika kiutaalamu
• Downer Cow ni yule ng’ombe anayeshindwa kusimama baada ya kutibiwa na Calcium borogluconate
| JINA LA TATIZO | SABABISHO | DALILI ZINGINEZO | TIBA |
| 1. Milk fever | – upungufu wa Calcium mwilini (Hypocalcaemia) | – Kuacha kula
– Kutochangamka
– Kupindisha shingo
– Joto la kawaida
| – Calcium boroglyconate |
| 2. Ketois | – Upungufu wa glucose
(Hypoglycaemia)
| – Kula kama kawaida
– Kuchangamka
– Joto la kawaida
| – Glucose
– Dextrose
– Oligovit
|
| 3. Vagina trauma | – Kuvuta ndama kwa nguvu (Dystocia) | – Kuacha kula
– Vidonda mkwaruzo ndani ya uke
– Homa
| – Antibiotics
– Oligovits
|
| 4. Coxo-femoral joint luxation | – Kuteleza | – Kula kama kawaida
– joto la kawaida
| – TLC
– Rekebisha joints
|
| 5. Acute mastisis | – Vijidudu kama bakteria | – kuvimba kiwele
– maziwa kubadilka rangi
– Homa
| – Antibiotics
– chinja
|
| 6. Obturatory nerve paralysis | – Kuvuta ndama Kwa nguvu (Dystocia) | – Kula kama kawaida
– Joto la kawaida
| – TLC
– Chinja
|
