Sasa


SIFA ZA BANDA BORA LA KUKU I Mshindo media

https://www.animalscience.care/

SIFA ZA BANDA BORA LA KUKU
Ukiamua kufuga katika banda kwa njia mbili
zilizoelezwa awali utatakiwa kujenga banda lenye
sifa zitakazokidhi mahitaji ya msingi ya kuku. Banda
bora la kuku linatakiwa kuwa kama ifuatavyo:
Liwe jengo imara
❖ Pasiwe na sehemu zilizo wazi kwenye msingi
na kati ya ukuta na paa. ❖ Banda lijengwe na vifaa vinavyopatikana
katika mazingira yako ili liwe na gharama
utakayoweza kumudu.
❖ Unaweza kutumia matofali ya udongo,
udongo, miti, fito,n.k. Ukitumia fito au
mabanzi ondoa maganda ili kuthibiti mchwa.
❖ Jengo mara litazuia maadui kama panya,
vicheche, paka, nyoka na wezi kuingia ndani
ya banda na kuwadhuru au kuwaiba kuku.
Liwe rahisi kusafisha
❖ Kuta na sakafu visiribwe zisiwe na nyufa ili
kurahisisha kusafisha.
❖ Pia itadhibiti kusiwe na wadudu wa kujificha
katika nyufa kama papasi, viroboto n.k.
❖ Sakafu ya banda lazima iwekewe matandazo
kama pumba ya mpunga au maranda ya
mbao au mabaki ya mazao au nyasi kavu
kutegemeana na kinachopatikana kwa
urahisi katika mazingira yako.
❖ Matandazo haya husaidia kunyonya unyevu unaotokana na kinyesi cha kuku au maji yanayomwagika katika banda.
❖ Banda hubakia kavu bila kuwa na harufu mbaya na wadudu kama inzi hata vimelea vya magonjwa hudhibitiwa.
Eneo la nje kuzunguka banda kuwe na usafi wa kudumu. Hali ya usafi nje ya banda itafanya wadudu kama
siafu au mchwa na wanyama kama panya na paka
mwitu wakose maficho. Nje ya banda ndani ya uzio
kuwe na miti midogo na mimea mingine midogo
kwa ajili ya kivuli.
Ufugaji nusu huria
• Liwe na nafasi ya kutosha kwa kuku waliopo:
Kwa kawaida eneo la mita mraba moja hutosha
kuku wanne wanaotaga au kuku 8 wa nyama.
Nafasi ya mita mraba 1 inatosha vifaranga 16
hadi kufikia umri wa majuma manne.
• Liweze kuingiza hewa na mwanga wa kutosha:
Banda linaloweza kuingiza hewa safi na kutoka
ndani yake hubaki kavu. Harufu mbaya hutoka
na kuku huweza kupumua hewa safi. Hii
husaidia pia kudhibiti kuzaliana kwa vimelea
vinavyosababisha magonjwa,hivyo hudhibiti
magonjwa.
Lisiwe na joto sana au baridi sana. Panda miti ya
kuzunguka banda lako ili eneo liwe na kivuli cha
kutosha na pia lisiwe na upepo mkali.Kama hali
halisi ya eneo la kufugia ina joto kubwa kwa vipindi
virefu paa la banda wakati wa ujenzi liinuliwe juu
zaidi kuruhusu mzunguko zaidi wa hewa na joto la
paa ( kama ni la bati) liwe mbali juu ya kuku. Joto
kwenye banda linaweza kusababishwa na
msongamano wa kuku, hivyo mfugaji aangalie
aweke idadi ya kuku inayowiana na ukubwa wa
banda lake.
PAA
Liwe imara na lisilovuja. Waweza kutumia mabati,
nyasi, madebe, makuti n.k. kutegemeana na
upatikanaji wa vifaa vya kuezekea.Wakati wa
kuezeka paa lisiishie karibu sana na ukuta bali liwe
na sehemu kubwa iliyozidi ukuta kuzuia mvua
kuingia ndani kama ni ya upepo ( angalia mchoro
hapa chini).
Kuku wakifugwa kwa mtindo wa nusu ndani na
nusu nje wanahitaji huduma mbalimbali ndani ya
banda na ndani ya wigo. Ili kutoa huduma hizi vifaa
vifuatavyo ni muhimu viwe katika banda:
Kuna njia nyingi za kutengeneza vyombo vya
kuwekea maji ya kuku ya kunywa.
• Aina ya mojawapo unayoweza kutumia ndoo au
debe la lita kumi au ishirini ya plastiki. Kata
ndoo hiyo pande nne kutoa nafasi ya kuku ya
kunywea kama kielelezo kinavyoonyesha.
Tengeneza idadi ya vyombo hivi inayowiana na
wingi wa kuku ulionao.
• Au waweza kutumia sufuria au beseni pana
kiasi. Hii huwekewa tofali au jiwe safi pana
baada ya kuwekewa maji ya kunywa ili kuzuia
kuku wadogo wasizame na maji yasichafi liwe
kirahisi.
• Vifaa maalum vya kunyweshea kuku
vinapatikana katika maduka ya pembejeo za
kilimo.
Vyombo vya Chakula Vyombo hivi ni muhimu viwe vimetengenezwa
vizuri ili visiwe chanzo cha upoteaji wa chakula.
Unapotengeneza kilishio cha kuku kumbuka kuwa
kuku wana tabia ya kuchakura. Husambaza au
kupekua chakula kwa miguu hata kwa midomo ili
kupata chakula cha chini.
Tabia hii husababisha kumwagwa kwa chakula kingi
chini na kusababisha hasara. Unaweza kudhibiti
tatizo hili kwa kutengeneza vyombo visivyoruhusu
kuku kuchakura kama inavyoonyeshwa kwenye
kielelezo hapa chini. Unaweza kutengeneza kilishio
hiki wewe mwenyewe au fundi seremala waliopo
katika eneo unaloishi. Inafaa kilishio kiwe
chembamba ili kuku wasiweze kuingia. Pia
kinatakiwa kiwe kirefu ili kuku waweze kula bila
kusongamana.
VIOTA Zipo aina tofauti za viota ambazo hutumika kwa ajili
ya kutagia. Ipo aina ya ambayo ni ya kutagia kuku
mmoja mmoja. Vipimo vinavyopendekezwa kwa kila
kiota ni upana wa sentimita 30, urefu sentimita 30
na kina sentimita 35. Upande wa mbele uachwe
wazi Kilishio Kinywesheo cha kujitengenezea
Kinywesheoila sentimita 10 za kwanza kutoka chini
zizibwe na ubao (angalia kielelezo). Weka idadi ya
viota inayotosheleza kuku ulio nao.
Pia ipo aina nyingine inayoweza kutumiwa na kuku
zaidi ya mmoja kwa wakati mmoja. Ni kama kiota
kimoja kilichogawanywa katika vyumba kadhaa. Ila
kila chumba kina vipimo kama vya kiota kimoja
(angalia picha hapa chini).Aina hii ya kiota ina
upana wa sentimita 30 na kina sentimeta 35 na
urefu wake unategemea idadi ya viota.
Viota vinatakiwa kuwa na giza ili kuku wasiogope
kuingia kutaga ndani yake. Pia giza husaidia
kupunguza tabia ya kuku kula mayai na kudonoana.
Kiota kinafaa kuwekwa mahali ambako ni rahisi
kuku kuingia na kutoka. Vile vile iwe ni sehemu
itakayorahisisha usafishaji wa kiota chenyewe.
VICHANJA Kuku wana asili ya kupenda kulala au kupumzika
sehemu iliyoinuka. Hivyo ndani ya banda weka
vichanja vitakavyotosheleza idadi ya kuku waliopo.
............................................................
Previous Post Next Post