Sasa


Uwiano wa joto kwa Vifaranga I Mshindo Media

https://www.animalscience.care/
Joto ni muhimu kwa ajili ya uhai wa
vifaranga. Ni
vyema joto la vifaranga likawa kama ifuatavyo:
        Wiki                  Joto (°C)  
1                  35
2                  33

3                  31
4                  29  

 5                  27
Katika sehemu za joto, vifaranga watakuwa
katika joto kwa wiki 2 tu. Ikiwa huna kipima joto
unashauriwa uangalie tabia na mwenendo wa
vifaranga wako
1: Kama vifaranga wamechangamka na kunywa
maji vizuri na wametawanyika sehemu zote joto
linatosha
2. Kama joto halitoshi vifaranga hujikusanya
karibu na taa au jiko ama chungu cha joto ama
chemli au hujirundika sehemu moja. Hivyo
unashauriwa kuongeza joto kwa kuongezea idadi
ya vifaa au nguvu ya joto mfano umeme au mkaa
3. Ikiwa joto ni kali sana, utaona vifaranga
wanakaa mbali na chanzo cha joto, wanatanua
mabawa, hulewa na kulala chini
...................................................................................................

Previous Post Next Post