Makundi ya vyakula:
- Vyakula vya kutia nguvu:
Vyakula vya mifugo vifuatavyo vinawekwa katika kundi hili;
a. Pumba za mahindi, pumba laini za mpunga, na, pumba laini za ngano.
b. Nafaka kama vile mtama , chenga za mahindi ,chenga za mchele, uwele , na ulezi
c. Mimea
ya mizizi kama vile muhogo, viazi vitamu na magimbi. Kabla ya kulisha
kuku hakikisha mizizi hiyo inalowekwa kwa muda wa saa moja au kupikwa
kabla ya kukausha ili kuondoa sumu ambayo kwa asili imo katika vyakula
vya aina hii.Inashauriwa kuwa mizizi hiyo ilishwe kwa kiasi cha
asilimia 10% ya chakula chote anacholishwa kuku.
Katika kundi hili la kutia nguvu ,vyakula vya mafuta
kama vile mafuta ya kutoka kwenye vyakula vya mafuta kama mashudu ya
mimea ya mafuta, mafuta ya samaki husaidia kuongeza nguvu na joto
mwilini. Vyakula vya kutia nishati huchangia asilimia 60-70 ya
mchanganyiko wote wa chakula.
1. Vyakula vya kujenga mwili:
Mashudu
:Haya ni makapi ya mbegu za mimea aina ya mikunde na vyakula v
vinavyotoa mafuta kama vile alizeti, mawese, karanga, soya ,korosho, na
ufuta .
Damu
ya wanyama iliyokaushwa (waliochinjwa na kukaguliwa), hii inafanywa ili
kuepusha uwezekano wa kuku kupata magonjwa ya kuambukiza .
Mabaki ya samaki ya samaki/dagaa na nyama.
Vyakula
asilia kama vile minyoo, mayai ya mchwa, Masalia ya nyama toka kwenye
ngozi/mifupa, wadudu walioteshwa kutokana na damu au nyama iliyooza na
vyakula vya aina nyingine.
Vyakula hivi huchangia asilimia 20 hadi 30% ya mchanganyiko wote wa chakula cha kuku.
2. Vyakula vya kuimarisha mifupa(madini): a)Hivi
ni vyakula vya madini ambavyo huhitajika kwa ajili ya kujenga mifupa,
maganda ya mayai, kukua na kuuweka mwili wa ndege (kuku) katika hali ya
afya njema kwa ujumla.
b) Madini
ya muhimu ni madini ya chokaa (calcium) na fosiforasi (phosphorus). Ili
kuku watage mayai yenye ganda gumu ni lazima wapate madini ya chokaa
maganda ya konokono na mayai yaliyosagwa vizuri. Lakini inapendekezwa
kwamba unapoongeza madini ya fosforasi inakubidi uongeze pia madini ya
chokaa kadri inavyopasa ,kwasababu kiwango cha aina moja kikizidi kuliko
cha aina nyingine husababisha upungufu wa kile kidogo
Viinilishe vya madini vinavyotakiwa ni pamoja na;
Majivu
ya mifupa yaliyosagwa vizuri, unga uliosagwa wa magamba ya konokono wa
baharini, konokono wa nchi kavu na maganda ya mayai yaliyochomwa . Kabla
maganda ya mayai na nyumba za konokono havijatumika inashauriwa
yachomwe moto mkali au yachemshwe ili kuua vijidudu vya maradhi.
Chumvi ya jikoni
Madini yaliyotengenezwa viwandani kama vile Di-calcium phosphate
Magadi (kilambo).
4. Vyakula vya kulinda mwili:
Kundi hili linajumuisha vyakula vya mbogamboga kama vile;
Ø Mchicha, samadi ya ng’ombe ambayo haijakaa muda mrefu baada ya kunyewa, mchicha pori, Chinese kabeji n.k.
Ø na Mchanganyiko wa vitamini uliotengenezwa na viwanda vya madawa (vitamin premix).
Ø Jua
ni muhimu katika kuhakikisha vitamini A na D zinatumika vizuri mwilini,
kwahiyo banda ni lazima lijengwe kwa mtindo ambao unaruhusu mwanga
kupita hasa nyakati za asubuhi na jioni.
Ø Chakula cha kuku wanaofugwa ndani ni lazima kichanganywe na vitamini zinazotayarishwa viwandani.
KUCHANGANYA CHAKULA CHA KUKU:
Njia za kuchanganya chakula cha kuku;
Kuna njia kuu mbili za kuchanganya chakula cha kuku, nazo ni;
Kuchanganya chakula kwa mashine;
o Njia hii hutumika viwandani kuchanganya chakula kwa ajili ya kuku wanaofugwa katika mashamba makubwa.
Kuchanganya chakula majumbani (home made ration): Hii
ni njia inayotumika kuchanganya chakula kwa ajili ya kulisha kundi dogo
la kuku na njia ambayo inaweza kutumiwa na wafugaji wadogowadogo.
VIFAA; Beleshi /koleo(spade), Turubai/sakafu safi, Viinilishe , Viroba/Magunia kwa ajili ya kuhifadhia chakula kilichochanganywa.
Chakula kilichochanganywa kinaweza kuwekwa katika uzani wa kilo 25-kilo 50, au kilo 100.
Aina ya chakula kiasi
i. Vyakula vya kutia nguvu mwilini:
Ø Pumba za mahindi kilo 48
Ø Pumba laini za mpunga kilo 26
Jumla kilo 74
ii. Vyakula cha kujenga mwili :
Mashudu ya alizeti kilo 18
Damu ya wanyama kilo 1
Mabaki ya samaki /dagaa kilo 3
Jumla kilo 22
iii.Vyakula vya kuimarisha mifupa (Madini):
- chumvi ya jikoni kilo ½
- chokaa(dicalciumphosphate)… kilo 2
- poultry premix/ kilo ½
- unga wa mifupa kilo 1
Jumla kilo 4
Ø Mahitaji halisi ya viinilishe kwa muhtasari:
Ø Vyakula kutia nguvu mwilini kilo 74
Ø Vyakula vya kujenga mwili kilo 22
Ø Vyakula vya kuimarisha mifupa (Madini) kilo 4
JUMLA 100
Jumla ya mchanganyiko wa vyakula kilo 100
HATUA ZA KUCHANGANYA CHAKULA CHA KUKU:
HATUA YA KWANZA:
Katika hatua ya kwanza utaanza kuchanganya vyakula vya madini
Changanya , chokaa, chumvi na majivu ya mifupa pig mix vizuri - huu utauita mchanganyo Na.1
HATUA YA PILI:
Changanya mchanganyo huo na damu pamoja na samaki waliosagwa - huu utauita mchanganyo Na. 2
HATUA YA TATU:
Mchanganyo Na.2 uchanganye na mashudu vizuri ambao utauita mchanganyo Na.3.
HATUA YA NNE:
Mchanganyo Na.3 umwage juu ya rundo la pumba iliyochanganywa (pumba ya mahindi na pumba laini ya mpunga).
o Chukua beleshi /koleo safi lililo kavu na kulitumia kuchanganya rundo la chakula ili kusambaza viinilishe vizuri.
Mambo ya kuzingatia katika kulisha na kutunza chakula cha kuku:
a) Baada ya kuchanganya chakula kitawekwa kwenye viroba
au magunia na kutunzwa ghalani (stoo) hadi pale kitakapohitajika kwa
ajili ya kulisha kuku.
b) Hakikisha kuku wanapata lishe kadri inavyopendekezwa na wataalamu.
c) Chakula kilichochanganywa ni lazima kiwekwe sehemu
kavu ili kisiharibiwe na unyevunyevu kama vile kwenye chaga mabanzi
yaliyotandazwa juu ya mawe yalipangwa vizuri
d) Chakula kilichoharibika hakifai kulisha kuku kwani kinaweza kusababisha matatizo ya afya.
d) Chakula kilichochanganywa kinatakiwa kisikae muda mrefu baada ya kutayarishwa.
Vyakula vya ziada:
Ili kuhakikisha kwamba kuku wanapata viinilishe vya kutosha kuku wanaweza kupewa mchwa na mafunza.
Vilevile vitu mbadala aina ya nafaka vinavyopatikana hutegemea sana aina ya mazao yanayolimwa katika eneo husika.
Mbinu za kuotesha mchwa na funza: Funza
na mchwa ni chakula kizuri na rahisi chenye viinilishe aina ya protini
kwa kuku wanaofugwa kwa mfumo huria unaoboreshwa. Hata hivyo vyanzo hivi
vya chakula cha protini huchangia tu vile ambavyo kuku wanatakiwa
kupewa.
a. Inashauriwa uwape vifaranga hao funza na mchwa kwa sababu ndio wanaohitaji protini kwa kiasi kikubwa na cha kuaminika.
Funza na mabuu yanaweza kuoteshwa kwa njia rahisi na kutumika kuboresha chakula cha vifaranga.
c) Mafunza na mabuu yanaweza kuoteshwa kwa
kutumia damu, viungo vya ndani ya tumbo la ng’ombe pamoja na samadi ya
ng’ombe.
d) Chungu kijazwe maji theluthi moja ya ujazo wake,
inzi watakuja na kutaga mayai katika mchanganyiko ambao mafunza
walioteshwa wataanza kula mchanganyiko huo.
e) Baada ya hapo vitu hivi vyote vitachanganywa
pamoja katika chungu kimoja kikubwa ambacho kitaachwa wazi wakati wa
mchana na kufunikwa wakati wa usiku.
f) Siku tano baadaye maji yatajazwa kwenye mtungi
huo na mafunza yatakusanywa wakiwa wanaelea juu. Baada ya kukusanya
waoshe vizuri na maji halafu lisha kuku moja kwa moja.
g) Kumbuka kuweka chungu kinachooteshwa mafunza kuweka mbali na maeneo ya watu ili kuepuka harufu inayoweza kusumbua watu.
Makadirio ya chakula cha kuwalisha vifaranga 100/siku moja:
Umri (wiki baada ya kuzaliwa)
|
Idadi ya
vifaranga
|
Kiasi kinachotakiwa
Kwa siku moja(kilo)
|
1
|
100
|
1
|
2
|
100
|
1
|
3
|
100
|
2
|
4
|
100
|
3
|
5
|
100
|
4
|
6
|
100
|
5
|
Maelezo kwa ufupi kuhusu kulisha kuku:
Ni
vigumu kukadiria mahitaji ya chakula cha kuku wanaojitafutia chakula,
lakini inakadiriwa kuwa kuku mmoja mkubwa wa uzito wa kilo 1-2 anahitaji
chakula chenye uzani wa gramu 80-160 kwa siku kwa kuku wanofugwa ndani
lakini wale kuku wanafugwa kwa mfumo wa huria nusu huria mahitaji
yanakadiriwa kupungua hadi kufikia gramu 30-50 kwa siku .
Ifahamike
pia kuwa kiasi cha chakula hutegemea mahitaji kutokana na uzito na
uzalishaji, mfano kuku anayetaga na anayekua wanahitaji chakula kingi
zaidi ya wale ambao hawatagi au wamekoma kukua.
Hakikisha kuku wanawekewa chakula na maji safi kwenye vyombo safi na kubadilisha kila vitakapoisha.
............................................................................................................................................
