Breeds of Goats- BOER GOAT / MBUZI BORA WA NYAMA

Mbuzi wa Nyama
BOER GOAT - MBUZI BORA WA NYAMA

ASILI

Kiasili ni mbuzi wa Afrika ya kusini ingawa ndani yake kuna damu toka bara Ulaya na India, hii ndio Mbegu kubwa Zaidi ya mbuzi wa nyama ukilinganisha na wengine. Pia wanazalisha kiwango kikubwa cha maziwa ingawa wanafaa Zaidi kwa nyama.


RANGI

Wana mwili wenye rangi nyeupa na kichwani wana rangi nyekundu au hudhurungi (brown) ingawa wapo weupe kabisa au wekundu/hudhurungi kabisa na hii hutokea kwa 0.001%


UMBO

Wana umbo kubwa kufikia kilo 110-135 kwa madume


Kilo 90-100 kwa majike

Wana masikio yaliyolala kama mbuzi wa kinubi (Nubians)Mbuzi wa Nyama


UZAZI

Huwa wanazaa mapacha na huweza kuzaa mara 2 kwa mwaka

Majike ni wazazi na walezi wazuri wa watoto sababu wana maziwa ya kutosha

Watoto hukua haraka sana, na nia aina ya mbuzi ambao sio wakorofi(docile)

Kwenye baridi kali au joto kali huwa inawaathiri kwenye kubeba mimba
.........................................................................................................



Previous Post Next Post