UGONJWA WA NDUI YA KUKU... Huu ni ugonjwa wa kuambukiza na hutokea mara kwa mara. Ugonjwa huu husababishwa na virusi na hushambulia aina zote za ndege ( ikiwa ni pamoja na kuku na bata mzinga) isipokuwa bata maji.
Vifaranga ndio hushambuliwa zaidi na ugonjwa huu kuliko kuku wakubwa. Ugonjwa huu hauui kuku wengi lakin kuku walioambukizwa hupungua uzito na utagaji mayai hupungua kwa kuku watagaji.
Dalili za ugonjwa huu huonekana baada ya siku 21 tangu maambukizi. Mashambulizi kuzidi kwenye wiki ya tatu au nne. Ugonjwa huu hushambulia sehemu ambazo hazina manyoya. Wakati huanzapo vivimbe vidogo hutokea puani, mdomoni na miguuni. Kwa kawaida kuku waliopona au waliochnjwa huwa hawashikwi tena ugonjwa huu....
UENEZAJI
A. Ugonjwa huenea polepole katika kundi la kuku.
B. Ugonjwa husambazwa kupitia ngozi iliyojeruhiwa ambayo inaguswa na kuku wagonjwa.
C. Kwa kupitia nzi wanaonyonya damu kutoka kwa kuku walioambukizwa ugonjwa huu na kunyonya damu ya kuku wasio na ugonjwa huu.
DALILI
Ziko dalili za aina mbili:
A. Upele wa rangi ya njano unaonekana kwenye undu, mashavu na usoni. Mara nyingine hutokea chini ya mabawa na miguu. Upele huu unaweza kuwa mwingi au kidogo na kudumu kwa wiki tatu au nne.
B. Uvimbe wenye rangi ya njano hutokea mdomoni, baadaye kidogo kupona na kuacha kidonda. Baadaye pua na macho hushambulia hivyo kuku hutokwa mate ambayo baada ya muda hugeuka yakawa kama usaha; halafu hutumika kabisa macho na pua.
Hali hii hudhoofisha kuku kwani huwa hawawezi kula na mwisho we vifo hutokea....
.............................................................................................................................
Tags:
MAGONJWA