Habari ndugu mfugaji ni matumaini yangu haujambo.Mimi ni wa afya na leo twende tuka one jinsi ya kutumia mikoo kuatamishia mayai.Kuna wafugaji wengi wanahitaji kumiliki machine za kutotolesha Vifaranga. Lakini maeneo wanayo kaa ndio huwa changamoto kupatikana umeme au hali ya maisha kuwa ngumu na kushindwa kununua kitotolesheo.Sasa hapa twende tukaone ni jinsi gani ya kufanya na utawezaje:Kuna njia kama mbili au zaidi zinazo weza kufanikisha hili.Kwanza kabisa unatakiwa kununua yale makoo ya kienyeji yenye umbo kumbwa na sifa ya kuatamia vizuri.(Mikoo ni kuku majike walio zeeka)Unaweza nunua mikoo 5 na mitetea 5 Sasa twende tukazione hizo njia jinsi ya kufanya!!
NJIA YA KWANZA
Hii unaweza tumia hata wale kuku kabla hawajaanza kutaga. Kitu cha kufanya ni kukusanya mayai kutoka kwa wale tetea kisha unatafuta tenga na kuandaa viota vizuri.1. Utatengeneza idadi ya viota kutegemea na idadi ya mikoo ulio nao2. Mayai ulio andaa kwa ajili ya kuatamia utayaweka kwenye viota3. Usiku unawachukua mikoo na kuwa weka kwenye viota ulivyo weka mayai4. Kila mkoo utamuweka kwenye kiota chake5. Ukisha wa weka utawafunika na tenga
MATOKEO
Matokeo huwa ni kesho yake baada tu ya kuwa funika na tenga:1. Ukikuta wote wamelala kwenye mayai , wameyafumbata kama kuku anae atamia. Basi hapo jua na utegemee bada ya siku 21 kupata Vifaranga. Kitu cha muhimu ni kuwaweke maji na chakula ndani ya tenga , Maana utakapo wafunika ni vema kuwaacha bila kufunua tenga mpaka wazoee siku 5 au zaidi. Faida ni kuwa baada ya siku 21 utapata Vifaranga wengi kwa wakati mmoja hii itaku rahisishia kwenye kuwa tunza Baada ya hayo mayai kutotolewa siku ya kwanza tu watakavyo maliza unatoa Vifaranga na kuwawekea mayai mengini , hapo hauta pata shida kama mara ya kwanza ulivyo wafunika na tenga.2. Ukikuta kuna wengine wamesimama au kulala pembeni ya mayai jua huyo hafai katika njia hii ya kumuatamisha kuku hata kama hajaanza kutaga.
ZINGATIA:
Kila mtetea utamfunika pekeyake kwenye viota ulivyoandaa.
NJIA YA PILI Hapa katika njia hii ni ya kuwasubirisha , njia hii hutumika mikoo au mitetea wakisha anza kutaga.Mikoo ni kuku wazee inamaana wametaga na kuatamia mara nyingi na kwa kawaida kuku wa kienyeji huwa kuna muda wana stop kidogo sasa katika njia hii kama mikoo/ mitetea wamestop kutaga na walivyoanza kutaga wamepishana siku unatakiwa uwasubirishe.
Mitetea wakisha anza kutaga chakufanya wewe utawasubirisha ili siku ya kutotoa watotoe pamoja Vifaranga wengi.Kuwasubirisha Itakusaidia Wewe Urahisi Wa Kuwalea Vifaranga Wako Na Katika Kuwapatia chanjo na chakula .Unajua kuna wafugaji huwa wanapata changamoto sana katika kuatamisha kuku, unakuta Vifaranga wengine wanatotolewa leo, wengine baada ya siku 4, wengine baada ya wiki sasa hapo kwenye kuwapa chanjo inakuwa ni changamoto kwa mfugaji.
Sifa Za Kuzingatia Wakati Wa Kuchagua Mitetea:Wawe na:
- Umbile kubwa.
- Uwezo wa kutaga wakiwa na umri mdogo (miezi 6).
- Uwezo wa kustahimili magonjwa.
- Uwezo wa kukua haraka.
- Uwezo wa kutaga mayai mengi {zaidi ya 15 kwa mtago mmoja (clutch)}.
- Uwezo wa kuatamia na kuangua vifaranga wengi na kuwalea.
- _Umbo kubwa.
- _Miguu imara na yenye nguvu.
- _Kucha fupi.
- _Mwenye nguvu.
- _Machachari.
- _Upanga/kilemba kikubwa.
- _Tabia ya kupenda vifaranga.
åNjia zitumikazo katika kuchagua kuku wa kuendeleza kizazi:
- Kwa kuangalia kuku wenyewe kulingana na sifa zilizotajwa hapo juu.
- Kwa kufuatilia kumbukumbu za wazazi wa kuku unaotaka kuwachagua.
- Kwa kuangalia kumbukumbu za familia (wazazi, kaka na dada).
- Wakati muafaka wa kuchagua kuku wa kuendeleza kizazi:
_Mara tu wakitotolewa. __Wakati wa ukuaji. __Zoezi endelevu.
_Uzalishaji ukishuka chini ya asilimia 50.
_Wakati kuku wanapoangusha manyoya.
Faida ya kuondoa kuku wasiofaa kwenye kundi:
- Inasaidia kuongeza uzalishaji wa mayai.
- Inapunguza kulisha kuku ambao uzalishaji wake ni hafifu
- Inapunguza uenezaji wa magonjwa ya kuku.
- Huongeza nafasi zaidi kwa kuku wazuri kwenye banda.
- Uwezekano wa kuuza kuku kama hao ni mkubwa kabla hawajafa. ............................................................