2. Sakafu ya nyavu za waya ni nzuri zaidi ila hakikisha hakuna sehemu
zenye ncha kali inayoweza kuwaumiza sungura, kwani wakumia ni mpaka
wapone wenyewe au umchinje kwa sababu ukitumia dawa za antibiotic
sungura hana uwezo wa kuzimeng’enya na kuisha mwilini mwake, siku
ukimchinja atabakia na dawa na hata ukinusa nyama yake utahisi harufu ya
dawa
3. Ukubwa wa banda usipungue mita 4 * 2 kwa kila sungura mmoja, likiwa kubwa zaidi ni vizuri
4. Chini kuwekewe matandazio kama nyasi kavu au maranda ya mbao, lakini
maranda yatokanbayo na miti yenye mafuta kama mi-pine na mikaratusi
hayafai, wawekee kipande cha blanket au taulo la zamani kwa ajili ya
kulalia na kujifungulia hasa kwa wazazi
5. Ni muhimu kuwawekea sehemu ya kujificha mara wanapohisi hatari, unaweza kutumia mbao, box gumu au plastiki.
UFUGAJI WA NJE
1. Sehemu yote izungushiwe wavu wa kuku kuzuia panya kuingia na wanyama wengine kama paka, mbwa, mwewe nk
2. Upande mmoja uwe na mabanda, sehemu ya chakula na maji pamoja na kivuli kwa ajili ya sungura kupumzika
3. Futi moja chini ya udongo kuwe na zege kuzuia sungura kuchimba na kwenda mbali
4. Eneo la wazi liwe huru na hatari zote za sumu kama dawa za kuulia
wadudu au mbolea, pia majani yaliyoota yasiwe ni yale yenye sumu (waone
wataalamu wakushauri au ng’oa yote)
MAJI
Tumia mabakuli ya kigae, plastiki au jengea kwa saruji, maji yabadilishwe kila siku na vyombo visafishwe kila siku.
CHAKULA
Wapewe majani, mabaki ya mboga za jikoni baada ya kuchambuliwa, pia
unaweza kuwawekea pumba au chakula cha kuku (growers mash) kwenye vyombo
maalum kama chakula chenye virutubisho (concentrates).
USAFI
Kila siku jaribu kuondoa uchafu kama vyakula vilivyo mwagika, na kinyesi
kilichoganda kwenya matandazio, fagia na kubadili matandazio angalau
mara moja kwa wiki, manyoya ya sungura
mzazi yasiondolewe hii huonyesha kwamba anakaribia kujifungua watoto.
MENO
Wakati mwingine meno ya mbele hukua sana na kumsababishia usumbufu
wakati wa kula, waone wataalam ukiona ni marefu zaidi na yanahitaji
kupunguzwa, dalili kuu ni sungura kushindwa kula kwa zaidi ya masaa 12.
MIGUU
Miguu ya sungura si kama ya wanyama wengine, nyayo zake zimefunikwa kwa
manyoya, angalia ukiona yananyonyoka kuna tatizo chunguza, kucha zake
nazi huhitaji kupunguzwa zikikua sana.
UBEBAJI
Usimbebe kwa kutumia masiki yake huwa wanaumia sana, shika ngozi nyuma ya shingo kama paka ukitaka kumbeba.
DAWA
Wapewe dawa ya minyoo kama piperazine kila baada ya miezi mitatu, dawa
za wadudu kama akheri powdeer zinyunyuziwe kwenya mabanda yao kuzuia
viroboto, usiwape dawa nyingine
bila ushauri wa kitaalamu, antibiotics ndio usijaribu kabisa kama nilivyosema mwanzo.
......................................................................................................................................................
Tags:
SUNGURA
