TARATIBU ZA CHANJO KWA KUKU

 Image result for kuku picha
TARATIBU ZA KUWAPA CHANJO KUKU
Mambo muhimu ya kuzingatia:
•Hakikisha unazingatia kwa makini masharti ya mtengenezaji wa chanjo: jinsi ya kuhifadhi, kutayarisha na njia inayotumika kumchanja kuku. Wakati wote zingatia masharti ya mtengenezaji kuhusu uhifadhi wa
chanjo ili isipoteze nguvu.
• Fuata ushauri wa daktari wa mifugo unapoandaa programu ya chanjo.
• Watoa chanjo wapatiwe mafunzo ya jinsi ya kutayarisha na kutoa chanjo
• Chagua aina ya chanjo kulingana na umri na hali ya kiafya ya kuku.
• Fanya usafi wa mara kwa mara katika mabanda ili kupunguza wingi wa vimelea kwenye mazingira.
• Tumia maji ambayo hayajawekwa dawa au kemikali kwa ajili ya kuchanganyia chanjo, k.m. maji ya kisima, mvua, n.k. Maji ya kuchanganyia chanjo yawe na ubaridi, yasiwe moto.
• Changanya chanjo kabla ya kutumia na iwekwe mbali na kuku.
• Pata ushauri wa daktari wa mifugo kabla ya kuchanja kuku wagonjwa au wale ambao hawako katika
muonekano mzuri
• Siku ya chanjo, usiwape kuku maji kwa masaa 3 – 4 ili waweze kunywa maji yaliyowekwa chanjo kwa
haraka.
• Zoezi la uchanjaji lifanyike haraka ili kupunguza usumbufu kwa kuku.
• Tenganisha kuku waliochanjwa na wale ambao hawajachanjwa.
• Baada ya kuchanjwa, kuku wawekwe kwenye banda linalopitisha hewa vizuri
• Baada ya kila zoezi la kuchanja, wafanyakazi wabadilishe mavazi, viatu/buti zisafishwe na kuwekwa dawa, na vifaa vilivyotumika viwekwe dawa ya kuua vimelea.
• Fuata utaratibu uliowekwa wa kuharibu/kusafisha vifaa vilivyotumika kuchanja
• Weka kumbukumbu za uchanjaji vizuri
Mambo ambayo hutakiwi kuyafanya unapochanja
• Kumwaga chanjo ovyo na kuchafua mikono au nguo
• Kuchanganya chanjo za aina mbili au zaidi, isipokuwa pale tu mtengenezaji wa chanjo atakavyoagiza
hivyo, au kwa ushauri wa daktari wa mifugo.
• Kutumia chanjo iliyopita muda wake
• Kutumia chanjo iliyobaki ili itumike kwa kazi ya siku nyingine
• Kuchanja kuku ambao wamepatiwa dawa aina ya antibiotiki.
• Kuchanja zaidi ya chanjo moja kwa wakati, iwapo haikuagizwa hivyo

....................................................................................................................
Previous Post Next Post