KUANZA UFUGAJI NGURUWE
Unapoamua kufuga nguruwe ni muhimu kujiuliza maswali kadhaa, kama:
Je kweli una nia ya dhati ya kufuga nguruwe?
Mahitaji na matakwa ya soko, aina ya nguruwe itakayokufaa, upatikanaji wa chakula na bei zake, utaaluma wa ufugaji ulionao?
Mfumo gani wa ufugaji unaofaa kwenye mazingira na mtaji ulionao?
Aina ya nyumba ya nguruwe inayokufaa na inayokidhi haja ya mazingira uliyonayo?
Uanze na nguruwe wangapi na wa aina gani?
Je kwa hela nilizo nazo zinatosheleza kuwafuga nguruwe mpaka nitakapoanza kupata mazao na kuyauza?.
Je kama hazitoshi nitafanyaje?

Utunzaji wa Nguruwe
i. Nyumba/makazi ya nguruwe
■ Nyumba ya nguruwe ni kati ya mambo muhimu kwenye uwekezaji na ufugaji wa nguruwe.
■ Kiasi cha nguruwe unachotaka kufuga, rika la nguruwe kwa mahitaji mbalimbali na mfumo wa ufugaji wa nguruwe unaotaka kuufuata ni baadhi ya mambo muhimu yatakayo kuongoza kuamua aina ya nyumba itakayofaa kuchagua

Sifa za banda bora
Sakafu:
Inashauriwa kuwa na sakafu bora na Hivyo basi sakafu iliyotengenezwa kwa saruji na yenye mwinuko (slope), au Mabanzi imara inaweza kutumika

Kuta:
Kuta za mabanda ya nguruwe zinatakiwa kuwa imara, ziwe na uwezo wa kuwasitiri nguruwe wasitoke nje
Kuta zinweza kutengenezwa kutumia vifaa vya ujenzi vinavyopatikana kwa urahisi kwenye eneo unaloishi ili mradi tu uzingatie uimara na udhibiti wa Hivyo basi vifaa kama mabanzi, fito au matofali yanaweza kutumika

Paa:
Paa ni muhimu sana kwa nguruwe ili kumsaidia kuhimili mabadiliko ya hali ya hewa mfano kumkinga nguruwe na jua au mvua kwani nguruwe wanauwezo mdogo wa kustahimili mabadiliko ya hewa kwa sababu ya kutoweza kutoa jasho vilevile mwili wake kuwa na mafuta mengi.
Paa liwe na urefu wa kutosha ili litoe nafasi ya kuingiza hewa ya kutosha ndani ya banda hasa kama ukuta umezibwa (solid walls)
Hivvo basi paa linaweza kupauliwa vizuri kwa nyasi, makuti, bati nk
Banda lililopauliwa vizuri kwa nyasi lina uwezo wa kuhifadhi hali nzuri ya hewa ndani ya banda ila haliwezi kudumu kwa muda mrefu.
Paa la bati kama likipauliwa vibaya halina uwezo wa kuhifadhi mazingira mazuri ya Lakirn kama likipauliwa vizuri Imaweza kuhifadhi mazrngira mazuri na kudumu kwa muda mrefu.

Mfumo wa kuondolea mkojo na kinyesi
Unapotengeneza banda la nguruwe hakikisha unaweka mfumo mzuri wa
kuondoalea mkojo na kinyesi. Vilevile hakikisha kuwa mkojo na kinyesi
hakitapakai ovo ovo kwani inaweza kuwa chanzo cha kueneza magonjwa hasa
minyoo.
Zingatia haya unapotaka kuanza mradi ufugaji nguruwe
Mambo muhimu ya kuzingatia wakati wa kutafuta/kununua nguruwe kwa ajili ya ufugaji ni
Lengo la ufugaji ambalo litakusaidia kubaini aina ya nguruwe watakaofaa
Ni vyema kununua nguruwe toka kwenye shamba au mfugaji mwenye sifa ya kuwa na nguruwe wazuri, na ambalo halina taarifa mbaya ya magonjwa n.k.
Tafuta taarifa na ikiwezeka na fanya ukaguzi wa shamba unaIotaka kununua nguruwe

Utunzaji nguruwe makundi mbalimbali
Huduma na matunzo ya watoto wa nguruwe
Huduma na matunzo ya watoto wa nguruwe
1. Huduma na matunzo kwa nguruwe anayekaribia kuzaa
Matayarisho ya chumba cha kuzalia
_Hakikisha kuwa chumba cha kuzalia kina nafasi ya kutosha
_Fanya marekebisho na ukarabati muhimu kama vile kukarabati sehemu zilizobomoka au sehemu kuukuu
Usiache sehemu kwenye chumba hicho zitakazoruhusu watoto vya nguruwe kutoka nje ya banda
_Hakikisha mazingira ya ndani ya banda ni safi.
_Tenga sehemu ndogo ndani ya banda kwa ajili ya watoto kujihifadhi
_Hakikisha kuwa hiyo sehemu inaweza kutoa hifadhi ya watoto dhidi ya baridi
_Unaweza kuweka matandiko (beddings) kama majani makavu, maranda n.k ili kujenga mazingira ya joto kwa ajili ya watoto
_Kama mama nguruwe alikuwa akikaa kwenye banda jingine ambalo halikuwa maalum kwa ajili ya kuzalia, utahitajika kumweka kwenye banda hili wiki moja kabla ya kuzaa

2. Wakati wa kuzaa
Wakati wa nguruwe kuzaa usisumbue zoezi la kuzaa kama mchakato
unaendelea vizuri. Unachotakiwa kukifanya ni kusimamia na utoe msaada
kwa mama nguruwe tu kama kuna tatizo
Baada ya kuzaa usiwatenge watoto na mama yao
Kata vitovu vya watoto kiasi cha sentimita 3 hadi 5 kwa wembe mpya au kikatio kilicho safi na kilichochemshwa
Paka madini ya joto (tincture of iodine) kitovuni
Hakikisha watoto wote waliozaliwa wananyonya kwa mama yao maziwa ya mwanzo (colostrum)
Wasaidie watoto wadhaifu waweze kunyonya

3. Huduma nyinginezo baada ya kuzaliwa
_Wapatie watoto madini ya chuma ndani ya wiki ya kwanza ya
kuzaliwa hasa siku ya tatu ya kuzaliwa. Hii ni muhimu kwa sababu madini
ya chuma ni muhimu kwa ajili ya kutengeneza damu.
Lakini maziwa ya mama nguruwe yana upungufu mkubwa wa madini ya chuma, vilevile watoto huzaliwa wakiwa na kiwango kidogo sana cha madini haya. Kutompa madini ya chuma kutaathiri ukuaji, ustahimilifu magonjwa na hatimaye kusababisha vifo
_Kata meno yaliyochongoka ya watoto, hii itasaidia kuondoa uwezekano wa kumuumiza mama wakati wa kunyonyesha, vivile, kutoumizana wenyewe.

_Hasi hasa vidume ambavyo hutavihitaji kwa matumizi ya mbegu
Njia ya kuhasi inayotumika kwa watoto ni ile ya wazi (open method), wasiliana na mtaalam wa mifugo ili akusaidie kwenye shoghuli hii
Kuweka alama za utambuzi (identification). Unaweza kutumia njia ya kukata pembezoni mwa sikio (ear notching), au kuvika vitambulisho maalum kwenye sikio (ear tagging)

4. Kuwapatia watoto chakula maalum (creep feed)
Hiki ni chakula kigumu chenye mchanganyiko kamilifu wa viinilishe
na wanachopewa watoto wa nguruwe wakiwa na umri wa wiki ya pili hadi
wiki tatu
mahitaji ya watoto kipindi hiki ni makubwa kulinganisha na uwezo wa maziwa wanayonyonya kutosheleza mahitaji hayo
Hi itawasaidia watoto kuzoea chakula kigumu, kutosheleza mahitaji yao ya viini lishe, na hivyo huwawezesha watoto kukua kwa haraka

Kuwaachisha watoto kunyonya
Hili ni zoezi la kuwatenganisha watoto na mama yao
Zoezi hili halitakiwi kufanywa kwa Fanya taratibu na kwa makini ili kutowapa watoto mshituko
Wanatakiwa wazoeshwe kula vyakula vigumu taratibu kabla ya kuachishwa kama ilivyoelekezwa hapojuu
Watoto wanatakiwa waachishwe kunyonya kwa kuzingatia uzito wao na sio umri wao
Ni vyema kuwaachisha watoto kunyonya wakiwa na uzito wa kilo 9-11
Kama watoto wamelelewa vizuri watafikia uzito huo wakiwa na umri wa siku 58 (Takriban miezi miwili)
Kama watoto watakuwa na uzito chini ya kilo 9 kwenye umri wa miezi miwili inaashiria kuwa walipatiwa matunzo duni
Baada ya kuwaachisha watoto kunyonya wanatakiwa kupatiwa mahali pazuri pa kukaa, penye nafasi ya kutosha, na kuwe na vyombo vya chakula na maji
Usiweke kundi kubwa la watoto (mfano zaidi ya watoto watatu) uliowaachisha kunyonya kwenye banda moja. Ni vvema watengwe kati ya majike na vidume
Watoto uliowaachisha wanatakiwa kulishwa chakula kidogokidogo lakini kwa mara nyingi

VYAKULA VYA NGURUWE NA ULISHAJI
A. Utangulizi
Lishe ya nguruwe ni moja ya swala muhimu sana kwenye dhana nzima ya ufugaji wa nguruwe. Lishe inagarimu yapata asilimia sabini na hata zaidi ya garama zote za ufugaji wa nguruwe. Kati ya matatizo mengi yanayosababisha tija na ufanisi duni wa uzalishaji wa nguruwe yanatokana na lishe duni. Lakini kama nguruwe wakipatiwa lishe bora, tija na ufanisi wa uzalishaji utakuwa mkubwa hivyo kuongeza faida kwa mfugaji.

B. Faida za kulisha lishe bora kwa nguruwe
1. Lishe bora huharakisha ukuaji wa nguruwe na kupata uzito unaohitajika kwa kipindi kifupi.
2. Lishe bora hupunguza gha ra ma za ufugaji na hivyo kuongeza faida kwa mfugaji sababu nguruwe atahitaji kiasi kidogo tu cha chakula na atachukua muda mfupi kupata uzito mkubwa
3. Lishe bora itapunguza maambukizi ya magonjwa.
4. Lishe bora huongeza kiasi cha mayai yatakayoivishwa na mama nguruwe na hivyo kuongeza idadi ya watoto watakaozaliwa
5. Lishe bora huongeza kiasi cha maziwa yatakayotengenezwa na mama nguruwe kwa ajili ya watoto hivyo kuwafanya wawe na afya bora itakayo wawezesha wakue haraka na kupunguza idadi ya vifo kwa watoto.
6. Lishe bora inaongeza ufanisi wa madume ya nguruwe na hivyo kuongeza uwezo wa kupanda

C. Viini lishe muhimu kwenye lishe ya nguruwe
Chakula cha nguruwe kilichokamilika kinahitaji kuwa na mchanganyiko wa viini lishe vitano, navyo ni

1. Vyakula vyenye kutia nguvu mwilini(Wanga) k.m
Pumba za mchele, Pumba za mahindi, Pumba za ngano, Machicha ya pombe yaliyokaushwa, Mihogo, Viazi vitamu, viazi mviringo, Ndizi mbichi, zilizoiva au zilizopikwa na makombo ya vyakula vya viasili vya wanga n.k

2. Vyakula va kujenga mwili (Protini) k.m
Mashudu ya alizeti, mashudu ya pamba na mawese, unga wa daga a/sa ma ki, da mu iliyokaushwa

3. Vyakula ay asili ya madini
Chumvi , chokaa ya mifugo (Limestone), mifupa iliyosagwa (bone meal), madini maalum ya nguruwe (Pig mix), madini mchanganyiko (k.m. maklic), madini ya chuma (hasa kwa watoto wa nguruwe) n.k.

4. Vyakula vya asili ya vitamini k.m
Majani mabichi laini, Mbogamboga, Matunda k.m parachichi, maembe, mapapai n.k, viungo mboga kama nyanya, bilinganya n.k. Michanganyiko maalumu yenye viasilia vya vitamini k.m. Vitamini premix n.k.

5. Maji
Hi ni lishe muhimu kwenye chakula cha nguruwe, ila tofauti na viini lishe vingine vilovyotajwa hapo juu ambapo nguruwe anapewa kwa vipindi/muda na kiwango maalum, maji yanahitajika kwa nguruwe muda wote.
............................................................................................................................................

Tags:
NGURUWE