MADHARA YA KUKU KUTAGA SEHEMU MOJA

 

Image result for kuku picha

Kuku kutagiana inamaanisha kuku wengi kutaga sehemu moja kwa muda tofauti tofauti

Hiki kitu huwa kinawatokea wafugaji wengi sana, Lakini pia kuna madhara ya kuku kutaga sehemu moja hasa kwa kuku kienyeji ambao wanaatamia.
  • Hii huwainatokea hivi kuku wa kwanza anavyo tafuta sehemu ya kutagia kipindi wenzake wana kuwa Bado hawajaanza kutaga kwa muda wa siku 4 au 5.
  • Baada ya kuku huyo kuanza kutaga inatokea kuku wengine wanataka waanze kutaga.
  • Kwa kuwa yule kuku wa mwanzo tayari amesha chagua sehemu ya kutagia na amesha anza kutaga kwa muda.
  •  Hawa wengine watakapo ona mayai ya mwenzao nao wataamua kutaga hapo hapo.
  • Madhara yanaanza kutokea wakati wa kuatamia yule kuku ambae ndio wa kwanza kutaga lazima atakuwa wa kwanza kuanza kuatamia huku wengine wa kiendelea kutaga.
  • Itafika kipindi kuku wote wanaanza kuatamia,  lakini kumbuka kuwa kuna kuku yule wa kwanza yeye aliwahi kuatamia kuliko wenzake.
  • Huyo kuku ni lazima atawahi kuatamia huku wengine wakiwa Bado.
  • Lakini kibaya Zaidi mayai ya huyo kuku  yatakapo anza kutotolea na hawa wengine watajua kuwa muda tayari umefika.
  • Na mwisho wa siku kuku wote huondoka kwenye kiota na Vifaranga wa chache wa mwenzao yule wa kwanza na mayai yao mengi huyaacha.
  • Kwahiyo hapo utaona jinsi gani kuna madhara ya kuku kutagiana. Mayai mengi huaribika .
JINSI YA KUDHIBITI
Mara tu utakapo ona kuku wengi wanatagia sehemu moja Fanya yafuatayo:
1. Waache watage sehemu hiyo bila kusumbua tena ikiwenzekana tengeneza kiota chao vizuri
2. Tafuta mayai viza  3 au 4 hayo mayai kayaweke hiyo sehemu wanapo taga
3. Andaa trey la kuwekea mayai na sehemu safi isiyo na joto
4. Kila siku watakavyo taga utakuwa ukikusanya mayai yote mazuri na kuwaachia Yale  viza ulilo yaweka ili waendelee kutaga
5. Mayaj yatunze vizuri kwenye trey sehemu yenye ncha ielekee chini, wakati wa kuyashika paka mikono majivu.
6. Katika kuku hao wanao taga ukiona kuna mmoja wapo anaonesha dalili ya kuanza  kuatamia, anakaa kwa muda mrefu kwenye kiota au ameanza kuyaatamia yale mayai viza uliyo yaweka.
7. Tengeneza kiota kingine chukua Yale mayai uliyo hifadhi tena chagua Yale ya siku za mwanzo kabisa, muwekee mayai kulingana na umbo lake. 8, 10 au Zaidi
8. Huyo kuku alie anza kuatamia utamuhamishia kwenye kiota ulichotengeneza, kwa siku za mwanzo utamfunika na tenga; hakikisha unampa maji na chakula
9. Utafanya hivyo kwa kuku wote na wataatamia vizuri kabisa pasipo shida yeyote
....................................................................................................................

Previous Post Next Post