Ufugaji wa Kuku wa Mayai
Misingi na taratibu za ufugaji bora
Tanzania
ni moja ya nchi za Afrika zinazokabiliwa na tatizo la ajira hasa kwa
vijana wengi wanao maliza elimu ya juu kuanzia ngazi ya astashahada hadi
shahada. Mfumo wa elimu yetu unatuhitaji baada ya kuhitimu, kijana
yampasa kuanza kutembea na bahasha zenye vyeti katika ofisi mbalimbali
ili kuomba nafasi za kazi. Hii pia inachangia sana kwa kiasi kikubwa
tatizo la ajira duniani.
Kwa
sasa takwimu zinaonesha kiwango cha ukosefu wa ajira kwa Tanzania ni
asilimia xxxx (xx%). Serikali imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali za
namna ya kupambana na tatizo la ajira Tanzanizia lakini binafsi bado
naamini tatizo la ajira litaondolewa na vijana wenyewe lakini hii
haimanishi serikali haina mchango wowote katika kutatua tatizo la jaira.

Vijana
wengi baada ya kuhitimu hawafikirii kutengeneza ajira badala yake
wanatumia mda mwingi kutafuta kazi za kuajiriwa ofisini kitu ambacho
kiuchumi kina athari kubwa. Baadhi ya vijana wamekuwa wakilalamikia sana
kuhusu tatizo la mitaji, ndio katika ufugaji mtaji ni mhimu sana katika
kufanikisha mradi wa ufugaji lakini mimi binafsi naamini katika wazo
yaani business plan yako maana hata wakati mwingine unaweza ambiwa
ukipewa hata millioni mia (100) utakuta huna wazo lolote la kuwekeza
hiyo millioni mia (100) ndo maana nasema mtaji sio tatizo kihiivyo bali
wazo ndo kitu mhimu na cha msingi.
Mwanzoni
mwa mwaka 2016 niliamua kuanza ufugaji wa kuku wa mayai amabapo
nilinunua vifaranga wapatao 1100 kutoka Malawi kwa aaajiri ya kuanza
ufugaji rasmi. Baada ya kuku wangu kuanza kutaga na kuona faida
inayopatikana na kupata ujuzi mbalimbali juu ya namna bora ya ufugaji wa
kuku wa mayai, nilipata msukumo mkubwa sana wa kuandika kitabu hiki
ambacho kitasaidia msomaji au mfugaji namna bora ya kufuga kuku wa
mayai.
Kitabu
hiki kinaeleza kwa undani kadri nilivyoandika jinsi ya namna ya ufugaji
bora wa kuku wa mayai. Kitabu hiki kinajumuisha maeneo makuu nane (08)
katika ufugaji wa kuku kuanzia siku ya kwanza ya kupokea vifaranga hadi
uuzwaji wa mayai ambayo ni: utangulizi, uandaaji wa banda la kuku,
Maandalizi bora ya upokeaji wa vifaranga wenye umri wa siku moja,
Mahitaji ya maji na chakula cha kuku, chanjo ya vifaranga na kuku,
utunzaji wa mahesabu na kukumbukumbu za mradi wa ufugaji wa kuku wa
mayai, utunzaji wa ubora wa mayai na masoko ya mayai na bidhaa
mbalimbali zitokanazo na kuku.
UANDAAJI WA BANDA LA KUKU
Kwa
kawaida na njia rahisi ufugaji wa kuku wa mayai hufanyika kwenye banda
yaani nyumba ya kuku. Banda hasa katika ufugaji mdogo wa kuku limekuwa
likitumika sana kwa mazingira yetu ya Tanzania na Afrika kwa ujumla.
Banda
la kuku wa mayai linawezwa kujengwa kwa kutumia mbao, miti, tofali za
kuchoma, mbichi au za saruji, au kwa kutumia mabati. Lakini kwa uzoefu
wangu ni bora banda lako lijengwe kwa kutumia tofali za kuchoma au za
saruji ili liwe na uimara zaidi.
Banda
lenye ubora ni lile ambalo linawapa usalama kuku wako wa mayai. Banda
lako hakikisha lina uimara zaidi ambao utazuia wezi kuingia ndani
kiurahisi, kuzuia nyoka kuingia ndani, ndege na wanyama wakali ambao
wanaweza kuathiri kuku wako.
Kwa
wastani ukubwa wa mita moja ya mraba ya banda inabeba kuku watatu (03)
kwa mujibu wa FAO lakini kwa uzoefu wangu mita moja ya mraba inaweza
kubeba hadi kuku watano (05), kwa hiyo unashauriwa kupima ukubwa wa
banda lako kulingana na idadi ya kuku wa mayai unaotegemea kufuga ndani
ya banda lako. Mara nyingi kwa uzoefu wangu ni bora banda lako moja liwe
na uwezo wa kubeba kuku mia tatu (300) maana hii itarahisisha utoaji wa
huduma ndani ya banda kwa maana ya utoaji wa maji, chakula na huduma
zingine kwa ufanisi zaidi.
Unapochagua
sehemu nzuri ya ujenzi wa banda lako hakikisha iwe rahisi kwako kupata
maji kwa ajiri ya kuku wako, chanzo cha joto na mwanga (mkaa, taa ya
chemri au umeme vitahitajika katika ufugaji wako), huduma za veterinary,
barabara nzuri zinazoweza kupitika kwa mwaka mzima hata kipindi cha
mvua, chakula cha kuku na soko la kuuza mayai na bidhaa mbalimbali
zitokanazo na ufugaji wa kuku kama vile kuku waliopunguza kiwango cha
utagaji na mbolea itokanayo na kuku.
Hakikisha
pia banda lako haliingizi maji ndani maana unyevunyevu ndani ya banda
la kuku ni mwiko kwa sababu bacteria wengi husababishwa na unyevunyevu.
Pia hakikisha banda lako haliingizi mwanga wa jua moja kwa moja ndani ya
banda lako la kuku maana mwanga wa jua wa moja kwa moja huathiri ukuaji
wa kuku wa mayai na hata utagaji pia.
Baada
ya kukamilisha banda lako hakikisha umelisakafia au umeweka zege ili
kutoruhusu bacteria ndani ya banda. Pia hakikisha banda lako umeliwekea
maranda ya mbao au maganda ya mchele. Binafsi napendelea sana kutumia
maganda ya mchele na nashauri kama unaweza kuyapata kiurahisi unaweza
kuyatumia nawe pia. Hakikisha unayaondoa baada ya kulainika na kuwa
mbolea, mbolea hii waweza uza au itumia shambani kwako hasa katika
kulimia mboga mboga ambazo pia hutumika kwa kuku wako ili viini vya
mayai wa kuku wako view vya kijani maana mayai ya aina hiyo hupenwa sana
na wateja.
Madrisha
ya banda lako yanapaswa kuwa makubwa ili hewa na mwanga (usiokuwa na
joto la jua) vipite kwa urahisi na kurahisisha mzunguko mzuri wa hewa
ndani ya banda. Banda lako liwe na madirisha pande zote mbili yaani
mbele na nyuma ili iwe rahisi kuruhusu hewa kutoka na kuingia ndani ya
banda. Madirisha yako yanaweza tengenezwa kwa mbao na kuwekewa nondo
ambazo si rahisi mtu kuingiza kicha ila kuzia wezi kuingia ndani ya
banda kiurahisi. Madirisha yako unaweza kuyawekea nyavu na pazia ambazo
zitashushwa kipindi cha usiku.
Eneo
la nje kuzunguka banda lako la kufugia kuku kuwe na usafi wa kudumu.
Hali ya usafi nje ya banda itafanya wadudu kama siafu au mchwa na
wanyama kama panya na paka mwitu wakose maficho. Nje ya banda ndani ya
uzio kuwe na miti midogo na mimea mingine midogo kwa ajili ya kivuli.
Banda
lako liwe rahisi kusafisha. Kuta na sakafu visiribwe zisiwe na nyufa
ili kurahisisha kusafisha. Pia itadhibiti kusiwe na wadudu wa kujificha
katika nyufa kama papasi, viroboto n.k. Banda lako liwe kavu mda wote na
lisiwe na harufu mbaya na wadudu kama inzi.
.........................................................................................................
.........................................................................................................
Tags:
KUKU WA MAYAI