FOWL CHOLERA (Kipindupindu cha kuku)
KIPINDUPINDU CHA KUKU
(Fowl Cholera)
Maelezo.
Ni ugonjwa wa kuku unaosababishwa na bacteria
ambao huenea kwa haraka na kusababisha vifo
vingi.
Ugonjwa hushambulia kuku na ndege wa aina zote ijapokuwa jamii ya bata huathirika zaidi kuliko kuku.
Jinsi Ugonjwa Unavyoenea
• Chanzo cha maambukizi ni hewa, maji na chakula
kilichochafuliwa na kinyesi cha kuku wagonjwa.
• Utupaji ovyo wa mizoga ya kuku, kwani mzoga
unaweza kukaa na vimelea kwa zaidi ya miezi mitatu.
• Kwa kawaida ugonjwa huanza kwa kuingiza katika
shamba/banda kuku wagonjwa kutoka nje. Baada ya
vimelea kuingia huenea kwa kupitia maji au vyakula
vilivyochafuliwa.
• Udongo uliochafuliwa na kinyesi cha kuku mgonjwa
huweza kuchafua maji na vyakula
• Hewa kutoka kwa kuku wagonjwa inaweza kuwa
chanzo cha maambukizi.
• Panya, ndege na wanyama wengine wanaweza
kueneza ugonjwa kwa kubeba mizoga ya kuku
waliokufa
kwa ugonjwa na kuchafua maji na vyakula.

Tahadhari: Wageni na wafanyakazi wanaweza
kusambaza ugonjwa kutoka shamba hadi
shamba au banda hadi banda
kusambaza ugonjwa kutoka shamba hadi
shamba au banda hadi banda
Dalili
Kuku wanaweza wasionyeshe dalili zozote za
ugonjwa, lakini dalili zifuatazo zinaweza kuonekana:
• Vifo vya ghafla vya idadi kubwa ya kuku waliokuwa
na afya
• Kuku wanakonda
• Kuku wanapumua kwa shida, wanakohoa na kupiga
chafya
• Uharo wa rangi ya kijivu, njano au kijani na
unaonuka
• Vifaranga wanaonyesha ulemavu
• Kuvimba magoti na kifundo cha mbawa
• Kichwa, upanga na undu hugeuka kuwa rangi nyeusi au zambarau
• Vifo vya kuku vinaweza kufikia asilimia 20
Uchunguzi wa Mzoga
• Madoa ya damu kwenye mapafu, utumbo na
kuzunguka moyo.
• Ini huvimba, laini na kuonekana kama limepikwa.
• Uchafu mgumu uliogandamana katika eneo
linalozunguka utumbo, kwenye masikio na machoni
• Pua na mdomo kuwa na makamasi mazito na
machafu

Kuzuia na Kinga
• Utaratibu ulio mzuri zaidi ni kuondoa kuku wote
kutoka kwenye shamba/banda ambalo ugonjwa
umethibitishwa, kupuliza dawa za viuatilifu kabla ya
kuingiza vifaranga na kuku wapya
• Mabanda yote ya kuku yapuliziwe dawa za viuatilifu
kabla ya kuingiza kuku wapya.
• Kuku wapya watenganishwe na kuchunguzwa kwa
muda wa angalau mwezi mmoja kabla ya
kuwachanganya na kuku wengine.
• Vifaranga visichanganywe na kuku wakubwa.
• Hakikisha unafuata kanuni za ufugaji bora ili kuku
wakue vizuri na wasiathirike.

TIBA
Ukiona dalili za ugonjwa huu wahi mapema kutumia
dawa mojawapo kati ya zifuatazo:

1. Tremazine
2. Typhoprim
3. Sulphonamides
4. Hipraloma
5.Ganadex
2. Typhoprim
3. Sulphonamides
4. Hipraloma
5.Ganadex
.....................................................................................................................................
Tags:
MAGONJWA