UMUHIMU WA KUFAHAMU VYANZO VYA MAGONJWA YA MIFUGO
Magonjwa mengi ya mifugo husababishwa na vyanzo kutoka nje ya mwili wa mnyama mfano; mazingira machafu anayoishi mnyama, vitu vinavyopelekea vidonda (vitu vyenye ncha kali) ambavyo husababisha vidonda na baadaye vimelea vinaweza kukaa.
Pia
mnyama anaweza kupata ugonjwa kutokana na hali za ndani ya mwili kama
upungufu wa lishe, mfano; madini na magonjwa ya kurithi.
Wadudu waenezi wa magonjwa ni kama vile;
Vimelea (bakteria)
Mfano wa magonjwa yanayosababishwa na vimelea ni kama vile chambavu, black quarter, kimeta, kifua kikuu, brucellosis, ugonjwa wa kiwele, na ng’ombe dume kuvimba mapumbu.
Virusi (virus)
Mfano wa magonjwa yanayosababishwa na virusi ni kichaa cha mbwa (rabies), ugonjwa wa midomo na miguu (foot and mouth disease) nansotoka (rinderpest).
Protozoa
Magonjwa yanayosababishwa na protozoa ni kama ndigana baridi, ndigana kali, ndigana mkojo damu na ndigama maji moyo na nagana.
Lishe duni
Upungufu wa viinilishe katika chakula cha mifugo husababisha madhara katika mwili kama ifuatavyo;
• Husababisha majike kutopata joto mapema
• Ndama kuzaliwa na viungo visivyokomaa
• Upungufu wa uzalishaji wa maziwa
• Kiwango cha uzalishaji kushuka.
Vidonda/michubuko
Kupitia vidonda au michubuko, wadudu wasababishao magonjwa huingia mwilini mwa mnyama na kuleta madhara.
Magonjwa ya kurithi
Kama
mmoja wa wazazi ana magonjwa au ugonjwa wa kurithi basi kuna uwezekano
mkubwa wa mmoja wa ndama watakaozaliwa kurithi ugonjwa huo.
Utunzaji bora wa afya ya mifugo
Uogeshaji
Mifugo
waogeshwe mara kwa mara ili kuepukana na magonjwa yaenezwayo na kupe
pamoja na ndorobo. Uogeshaji unaweza kufanyika kwa kutumia pampu za
mgongoni au kwa kuwatumbukiza katika josho lililotiwa dawa ya kuogesha.
Kuwapa dawa za minyoo
Mifugo
wapatiwe dawa za minyoo mara kwa mara ili kuhakikisha ukuaji wao na
utoaji wa maziwa uendelee vizuri. Mifugo wapewe dawa za minyoo kila
baada ya miezi mitatu.
Kuhasi
Ndama
dume wasiohitajika kwa ajili ya kuzalisha baadaye, wahasiwe kwa njia ya
upasuaji au kwa kutumia koleo au badizo iwapo ndama ni wakubwa.
Kuwapa ndama alama za utambulisho
Ndama
wapewe namba au alama za utambulisho mara wafikiapo miezi 6 tangu
kuzaliwa na utambulisho huu unaweza kuwa wa chuma au wa plastiki chenye
namba kwenye sikio.
Kuondoa vishina au vichomozo vya pembe
Ndama
waondolewe pembe katika mwezi wa kwanza tangu kuzaliwa kabla vishina
havijakomaa na kusababisha kushindwa kutoka kwa miezi ya mbeleni. Tumia
chuma cha moto kutoa vichomozo vyote vya pembe na hii husaidia ndama
kukua katika mwonekano mzuri na kutokuwa na pembe zinazoweza kuumiza
wenzake pindi ziwapo kubwa.
Kuondoa kwato
Kwato
za ndama ziondolewe miezi mitatu ya mwanzo, ili kusaidia kupunguza
kuondokana na magonjwa ambukizi ambayo husababishwa na kukatika kwa
kwato zikiwa kubwa pindi awapo malishoni au akiwa katika banda lenye
sakafu ya saruji.
..........................................................................................................
Tags:
MAGONJWA