Shubiri mwitu (Aloe VERA) ni mmea
ambao umekuwa ukitumika kwa kutibu magonjwa mbalimbali ya binadamu na mifugo.
Mmea huu unatumika sasa kutengeneza sabuni, dawa za binadamu na wanyama na
mambo mengine mengi.
Na kwa sababu ya madawa mengi ya kiwandani kushindwa kutibu
baadhi ya magonjwa kwa sababu wadudu wametengeza ukinzani, ipo haja kubwa ya
kuweka umuhimu kwenye madawa ya asili yatokanayo na mimea.
Mmea wa aloe vera unauwezo wa kutibu magonjwa ya kuku hasa
coccidiosis na kwa kiasi fulani Newcastle disease. Tafiti zilifanyika kwa
kutumia mti huu kutibu ugonjwa coccidiosis ambao mti huu unaweza kutumiwa kama
mbadala wa dawa za viwandani.
Maji maji ya mmea huu yanauwezo wa kutibu magonjwa na kuponyesha
majeraha yanayotokana na maambukizi ya magonjwa pamoja na kupandisha kinga ya
kuku kwa asilimia 50 dhidi ya maonjwa mbalimbali.Mmea wa aloe vera unaweza
kupandwa maeneo ya karibu na mabanda ya kuku ili kurahisisha upatikanaji wake
na unakubali maeneo karibu yote.
Majina ya mmea huu kulingana na baadhi ya makabila na kimataifa
Jina la Mmea/Name
|
Lugha/Language
|
Shubiri
mwitu
|
Kiswahili
|
Mkankiruri
|
Kinyaturu
|
Itembwe
|
Kigogo
|
Ibhata
|
Kinyiha
|
Litembwetembwe
|
Kihehe
|
Koli
|
Kikaguru/Kinguu
|
Aloe
|
Kiingereza
|
Aloe
vera
|
Kisayansi
|
Shubiri mwitu kwa ukuaji wa kuku Kulingana na tafiti zilizofanywa na Bejar (Chuo kikuu cha Kilimo na Misitu cha Samar) na Clapo (Chuo Kikuu cha Ufilipino Mashariki) inaonyesha kuwa ziada ya Shubiri mwitu kwenye maji inasaidia kwa kiasi kikubwa kuku kukua haraka.
Mililita 15 had 20 za maji ya shubiri mwitu yakichanganywa na
lita tano za maji kila siku kwa kuku 90 yanauwezo wa kusaidia ukuaji wa kuku na
kuongeza uzito wa ukilinganisha na wale ambao hawajapewa.
Shubiri mwitu (moja) inaweza kukatwe
vipande vipande na kulowekwa ndani ya maji ya kunywa kiasi cha lita 1-hadi 3
kutegemeana na idadi ya kuku. Viache humo kwa siku kadhaa hadi unapobadilisha
maji ndipo uviweke vingine. Ukiweza kuchuja mchuzi wa shubiri mwitu basi unakuwa
ukitumia mililita 15 ndani ya lita tano ya maji ya kunywa kuku kwa kuku 90 kama
unakuku wachache basi punguza kiasi cha dawa au ongeza kama ni wengi.
Kuku mwenye vidonda kama kwa ugonjwa
wa mdondo (Newcastle Disease) inakubidi utengeneze unga. Kata vipande
vidovidogo vya shubiri mwitu kisha changanya na pumba kidogo, vitwange na
kuvichekecha ili upate unga laini. Uanike na kisha tunza vizuri tayari kwa
kuutumia mara kuku wauguapo. Kuku wenye vidonda waoshwe vizuri kwa maji safi na
sabuni pamoja na chumvi kidogo. Baada ya hapo paka unga wa shubiri kwenye
vidonda hivyo.
.................................................................................................................................................................................
.................................................................................................................................................................................
Tags:
DAWA ZA MIFUGO
