Karibu mpenzi
msomaji wa blog hii ya Ufugaji na matibabu, nichukue nafasi hii kukushukuru
sana kuwa sehemu yetu, kwa kuwa mara kadhaa umekuwa unajifunza masomo
mbalimbali kupitia blog yetu hii, hivo niseme asante sana. Baada ya kusema hayo
machache naomba twende moja kwa moja katika somo letu la leo. Leo tutajifunza
kwa jinsi ya kujua yupi ni jogoo au tetea bora.
Mara nyingi wakati unafanya uchaguzi wa jogoo
kwa ajili ya kufuga ni lazima uangalie, jogoo ambaye atakuwa na sifa zifuatao;
1. SIFA ZA JOGOO BORA
- Awe na umbo kubwa.
- Awe na ushungi nzuri usioangukia upande mmoja.
- Awe mchangamfu.
- Apende kuwa na himaya yake. Sifa hii utaigundua pindi ukimjazia wapinzani, atakuwa anapigana badala ya kufuata matetea.
2. SIFA ZA TETEA BORA
- Awe na umbo kubwa.
- Awe na uwezo wa kuatamia.
- Awe na uwezo wa kulea vizuri (high mothering ability).
- Aweze kutaga mayai ya kutosha(profitability).
Tags:
MBINU ZA UFUGAJI
