UFUGAJI BORA WA BATA BUKINI
Kiasili bata bukini ni ndege ambao asili yao ni India na Japan. Hii ni jamii ya
ndege wafugwao lakini tofauti kubwa ya bata wa kawaida wao wana asili ya
usafi, hivyo hawapendi uchafu na kamwe hawali mizoga.
Tofauti
na ndege wengine au bata wengine wa kawaida, mfugaji wa bata bukini
anaweza kupata kipato kikubwa kwa haraka na kwa gharama ndogo
ukilinganisha na bata wengine.
Kuna
aina mbili ya bata bukini ambao ni weupe na wenye mchanganyiko wa
rangi. Hali kadhalika hutofautiana katika utagaji wa mayai.
Ndege
hawa wanakula chakula kama wanacholishwa kuku, wanapendelea kula majani
jamii ya mikunde kwa 50% na hawahitaji chakula kingi. Vifaranga ni
lazima wapatiwe lishe kamili hasa protini kwa wingi ili waweze kujenga
mwili, kukua vizuri na kuwa na afya nzuri.
Jitengenezee chakula cha bata bukini kama ifuatavyo:
Mahitaji kupata chakula cha bata 45kgs
1. Mahindi kilo 10 ( hakikisha hayana dawa)
2. Chokaa kilo 5 (ya kulishia mifugo)
3. Dagaa kilo 10 (wanaotumika kulishia kuku)
4. Mashudu kilo 20.
KUMBUKA;
Kiasi hiki cha chakula kinategemeana na wingi wa bata unao wafuga
Kuatamia
Bata bukini wamekuwa tofauti na ndege wengine
Bata
Bukini kutaga baada ya miezi saba na hutaga mara tatu kwa mwaka.
Isipokuwa, utagaji wa bata bukini weupe na wa rangi hutofautiana katika
idadi ya mayai, Bata Bukini weupe hutaga mayai sita tu lakini wale wa mchanganyiko wa rangi hutaga mayai kumi na mbili
. Bata Bukini weupe huatamia mayai 6 na wale wa rangi
huatamia mayai 12
Ndege
hawa huatamia kwa siku 29, huangua vifaranga kwa siku 3 na mara nyingi
hutotoa mayai yote, si rahisi mayai kubaki bila kutotolewa au
kuharibika.
Namna ya kutunza vifaranga
Mara
tu vifaranga wanapoanguliwa, wachukue na kuwatenga na mama yao kisha
waweke katika banda safi lisilopitisha baridi. Unaweza kuwawekea taa ya
umeme kama una uwezo ili kuwatengenezea joto.
Pia, waweza kuzungushia banda lao kitu kizito kama blanketi ili kuwakinga na baridi au upepo.
Banda
Bata Bukini wanahitaji nafasi ya kutosha hivyo andaa banda kulingana na wingi wa bata unaotarajia kufuga.
Hakikisha
banda limesakafiwa au banda la udongo lisilotuamisha maji au unaweza
kuweka mbao au mabanzi kisha unaweka maranda ili kuwakinga na baridi.
Maji
Ni
lazima bata wapatiwe maji ya kunywa kila siku na hakikisha banda
halikosi maji wakati wote. Safisha chombo cha maji na kubadilisha maji
kila siku.
Ndege
hawa wanahitaji maji ya kunywa ya kutosha kama ilivyo kwa kuku.
Hakikisha maji yako kwenye chombo ambacho hayatamwagika , kwani
kumwagika kunaweza kusababisha kuibuka kwa magonjwa. Bata Bukini
hawapendi uchafu. Hivyo maji yawe mahali ambapo hayatachafuka.
Magonjwa
Ni
mara chache sana bata bukini kushambuliwa na magonjwa kama watawekwa
katika hali ya usafi. Magonjwa yanayoweza kuwasumbua ni mafua na wakati
mwingine kuharisha.
Tiba za asili
Unaweza kutibu bata bukini kwa njia za asili. Tumia mwarobaini, vitunguu (maji na saumu).
1. Mwarobaini
Unaweza kutumia dawa hii kutibu mafua kwa bata bukini wakubwa au vifaranga.
Maandalizi
Chukua
kiasi kidogo cha mwarobaini kisha twanga vizuri kupata maji maji. Kamua
maji ya mwarobaini, kisha changanya na maji uliyo andaa kuwanywesha
vifaranga.
2. Kitunguu Saumu na Kitunguu Maji:
Dawa hii hutumika kukinga na kutibu bata bukini wanaoharisha.
Maandalizi
Unachukua
kitunguu saumu au maji na kuondoa maganda ya nje kisha safisha na
kukata vipande vidogovidogo na kuwawekea kama chakula.Unaweza kuwapatia
kila siku hadi watakapopona.
3. Majani: Bata
Bukini chakula chao kikubwa ni majani. Majani yana vitamini A, hivyo
hakikisha unawapatia ya kutosha. Wapatie majani jamii ya mikunde.