Kuna
aina nyingi za magonjwa yanayoshambulia nguruwe, lakini kuna magonjwa
ambayo yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara(common diseases) ambayo ni
lazima kukabiliana nayo ili kuwa na ufugaji
wenye tija na endelevu.
1. Ugonjwa wa miguu na midomo
Ugonjwa huu huathiri nguruwe sehemu za miguu na midomo. Ni ugonjwa ambao hushambulia nguruwe mara kwa mara hasa wasipokuwa na matunzo mazuri. Ugonjwa wa miguu na midomo, hudhoofisha nguruwe kwa haraka sana, ikiwa ni pamoja na kupungua uzito.
Chanjo: Chanjo kwa ajili ya ugonjwa wa midomo na miguu (FMD vaccine) hutolewa kila baada ya mwaka mmoja. Hii inasaidia kuwaweka nguruwe wako katika hali nzuri zaidi bila kushambuliwa na magonjwa hayo.
Tiba: Ugonjwa huu hauna tiba halisi. Inapotokea nguruwe wakawa wameshambuliwa kinachofanyika ni kutibu magonjwa nyemelezi kwa kutumia antibiotics.i.e Oxtetracycline
2. Homa ya Nguruwe (Swine fever)

Ugonjwa huu hutokana na virusi vinavyosababisha ugonjwa wa homa ya nguruwe huenea kwa haraka sana miongoni mwa makundi ya nguruwe, na huua kwa haraka sana, lakini hauna madhara kwa binadamuna hauambukizwi kwa binadamu. Nguruwe walioambukizwa waanshikwa na vindonda ama mapunye kwenye ngozi. Pia masikio na ngozi huwa mekundu. KUMBUKA
- Ugonjwa huu huweza kusambazwa na binadamu kwa kuhamisha mizoga toka sehemu moja kwenda nyingine
- Homa ya nguruwe ni lazima iwekewe karatini kwa sababu husambaa kwa haraka sana. Nchini Tanzania mlipuko wa homa ya nguruwe umekuwa ukitokea mara kwa mara maeneo ya mpakani mwa Tanzania na Malawi na katika mkoa wa Mbeya.
Chanjo: Ugonjwa
huu hauna chanjo wala tiba. Kinachofanyika mlipuko unapotokea ili kuwa
salama ni kuwateketeza nguruwe wote walioathirika na kuanza upya.
Unaweza kuteketeza kwa kuwachoma moto.
Muhimu: Baada
ya kuwateketeza nguruwe wagonjwa, safisha banda kisha nyunyiza dawa
aiana ya Acon au Ectomin wakati mwingine tumia V-RID, na uache banda wazi kwa kipindi cha wiki moja
kabla ya kuweka nguruwe wengine.
3. Ugonjwa wa mapafu (Pneumonia)
Huu ni ugonjwa unaoshambulia sehemu za koo na mapafu ya nguruwe, ambapo husababisha kukohoa na kupumua kwa shida. Ugonjwa huu husababishwa na bacteria, joto kupita kiasi, vumbi na gesi inayotokana na madawa makali.
Tiba: Homa ya mapafu kwa nguruwe inatibika kwa kutumia antibiotics. Pamoja na kuwaweka wanyama sehemu safi, isiyo na baridi kali au joto la kupitiliza kiwango.
4. Kimeta (Anthrax)
Huu ni ugonjwa unaosababishwa na bakteria wanaojulikana kama Bacillus anthracis,Bacteria hawa hubaki kuwa hai kwa muda mrefu na wanaweza kuwa kwenye udongo wakiwa hai kwa kipindi cha miaka mingi.
Chanjo: Chanja nguruwe wako dhidi ya kimeta kama utakavyoelekezwa na wataalamu wa mifugo walio karibu nawe.
Tiba: Unaweza kutibu nguruwe wako kwa kutumia dawa aina ya Penisilin au Oxytetracycline.
.........................................................................................

Tags:
MAGONJWA